Mtiifu, Tii, Utii Ona pia Amri za Mungu; Baraka, Bariki, Barikiwa; Shangwe; Sheria; Sikiliza; Tembea, Tembea na Mungu Katika maana ya kiroho, utii ni kufanya mapenzi ya Mungu. Nuhu alifanya kulingana na yote ambayo Mungu alimwamuru, Mwa. 6:22. Ibrahimu alimtii Bwana, Mwa. 22:15–18. Yote Bwana aliyosema tutayafanya, Ku. 24:7. Sikiliza kwa hiyo, Ee Israeli, na angalia uyafanye, Kum. 6:1–3. Mpende Bwana na ukatii sauti yake, Kum. 30:20. Kutii ni bora kuliko dhabihu, 1 Sam. 15:22. Mwogope Bwana na ukashike amri zake, Mh. 12:13–14. Si kila mtu ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba, Mt. 7:21 (3 Ne. 14:21). Kama mtu yeyote atayafanya mapenzi yake, atajua kama mafundisho haya ni ya Mungu, Yn. 7:17. Yatupasa kumtii Mungu zaidi kuliko wanadamu, Mdo. 5:29. Watoto, watiini wazazi wenu, Efe. 6:1 (Kol. 3:20). Nitakwenda na kufanya mambo ambayo Bwana ameamuru, 1 Ne. 3:7. Nilitii sauti ya Roho, 1 Ne. 4:6–18. Kama wanadamu watashika amri za Mungu, yeye atawalisha, 1 Ne. 17:3. Jihadharini msije mkaitii pepo mchafu, Mos. 2:32–33, 37 (M&M 29:45). Wanadamu huvuna thawabu zao kulingana na roho wanayoitii, Alma 3:26–27. Wanadamu yawapasa kufanya mambo mengi kwa ridhaa yao wenyewe, M&M 58:26–29. Wanadamu hawamkosei Mungu katika lolote, isipokuwa wale wasioukiri mkono wake na wasiotii amri zake, M&M 59:21. Mimi Bwana hufungwa mnapofanya yale nisemayo, M&M 82:10. Kila nafsi yenye kutii sauti yangu itauona uso wangu na kunijua Mimi ndimi, M&M 93:1. Watu lazima warudiwe hadi wajifunze utii, M&M 105:6. Tupatapo baraka yoyote kutoka kwa Mungu ni kwa sababu ya utiifu wetu kwa sheria ile ambayo juu yake hutoka, M&M 130:21. Adamu alikuwa mtiifu, Musa 5:5. Tutawajaribu ili kuona kama watafanya mambo yoyote yale ambayo Bwana atawaamuru, Ibr. 3:25.