Utawala Ona pia Katiba Yesu Kristo atakaporudi, ataanzisha utawala wa haki. Utawala utakuwa mabegani mwake, Isa. 9:6 (2 Ne. 19:6). Mpeni Kaisari vitu vilivyo vya Kaisari, Mt. 22:21 (M&M 63:26). Itiini mamlaka ya juu, Rum. 13:1. Salini kwa ajili ya wafalme na wote walio katika mamlaka, 1 Tim. 2:1–2. Wanyenyekeeni wenye himaya na mamlaka na kuwatii mahakimu, Tit. 3:1. Tiini kila sheria ya wanadamu kwa ajili ya Bwana, 1 Pet. 2:13–14. Yesu Kristo atakuwa ndiye msimamizi wa mwisho wa dunia, Ufu. 11:15. Wafanyeni watu wa haki wawe wafalme wenu, Mos. 23:8. Fanyeni mambo yenu kwa kura za watu, Mos. 29:26. Kristo ajapo atakuwa mtawala wetu, M&M 41:4. Yule ashikaye amri za Mungu hahitaji kuvunja amri za nchi, M&M 58:21. Waovu watawalapo, watu huhuzunika, M&M 98:9–10. Tawala zimewekwa na Mungu kwa manufaa ya wanadamu, M&M 134:1–5. Watu wana lazimika kuzikubali na kuziunga mkono serikali, M&M 134:5. Tunaamini katika kuwatii wafalme, marais, watawala na mahakimu, M ya I 1:12.