Barnaba
Jina aliopewa kwa Yusufu (pia aliitwa Yusufi), Mlawi wa Kipro, aliyeuza shamba lake na kutoa mapato yake kwa Mitume (Mdo. 4:36–37). Ingawa hakuwa mmoja wa Mitume Kumi na Wawili wa mwanzoni, alikuja kuwa Mtume (Mdo. 14:4, 14) na alikwenda katika safari kadhaa za kimisionari (Mdo. 11:22–30; 12:25; 13–15; 1 Kor. 9:6; Gal. 2:1, 9; Kol. 4:10).