Ustawi Ona pia Funga, Kufunga; Maskini; Sadaka, Utoaji sadaka; Utumishi Utaratibu na njia itumikayo kwa ajili ya kuwatunza watu kimahitaji ya kiroho na ya kimwili. Mfumbulie mkono wako nduguyo, maskini wako, na kwa mhitaji wako katika nchi yako, Kum. 15:11. Mtu awapaye maskini hatapungukiwa, Mit. 28:27. Je, hii siyo funga niliyoichagua? kuwapa wenye njaa mkate, kuwaleta maskini nyumbani mwangu, Isa. 58:6–7. Nalikuwa na njaa nawe ukanipa chakula; nalikuwa mgeni nawe ulinikaribisha ndani. Wakati umtendeapo mmoja wa ndugu zangu wadogo hawa, umenitendea mimi, Mt. 25:35–40. Mhudumieni kwa mali zenu yule mwenye shida, Mos. 4:16–26. Walipeana vitu vya kimwili na kiroho kulingana na shida na matakwa yao, Mos. 18:29. Waliamriwa kujiunga katika kufunga na kusali kwa ajili ya ustawi wa wale ambao hawakumjua Mungu, Alma 6:6. Sali kwa ajili ya ustawi wako na kwa ustawi wa wale wanaokuzunguka, Alma 34:27–28. Walikuwa na vitu vilivyo sawa miongoni mwao, 4 Ne. 1:3. Wakumbuke maskini, M&M 42:30–31. Watembelee maskini na wenye shida, M&M 44:6. Wakumbukeni katika mambo yote maskini na wenye shida, M&M 52:40. Ole wenu ninyi matajiri ambao hamtawapa maskini vitu vyenu, na ole wenu maskini ambao hamridhiki, na mlio wachoyo, na hamfanyi kazi, M&M 56:16–17. Katika Sayuni hapakuwa na maskini miongoni mwao, Musa 7:18.