Ufunuo wa siku za mwisho huzungumzia jehanamu katika maana zipatazo karibu mbili. Ya kwanza, ni mahali pa makazi ya muda katika ulimwengu wa roho kwa wale ambao hawakuwa watiifu katika maisha ya duniani. Katika maana hii, jehanamu ina mwisho. Roho hizo zitafundishwa injili, na wakati mwingine baada ya toba zao wataweza kufufuka katika daraja la utukufu ambalo watakuwa wanastahili. Wale ambao hawatatubu, lakini hata hivyo wao siyo wana wa upotevu, watabakia katika jehanamu wakati wote wa milenia. Baada ya miaka hii elfu moja ya mateso, watafufuliwa katika utukufu wa telestia (M&M 76:81–86; 88:100–101).
Ya pili, ni mahali pa kudumu pa wale wasiokombolewa kwa Upatanisho wa Yesu Kristo. Katika maana hii, jehanamu ni ya kudumu. Ni kwa ajili ya wale wanaopatikana kuwa “bado wachafu” (M&M 88:35, 102). Hapa ni mahali ambapo Shetani, malaika zake, na wana wa upotevu—wale ambao wamemkataa Mwana baada ya Baba Kumfunua kwao—watakaa hapo milele (M&M 76:43–46).
Maandiko wakati mwingine huitaja jehanamu kama giza la nje.