Misaada ya Kujifunza
Laani, Laana


Laani, Laana

Katika maandiko, laana ni matumizi ya sheria takatifu ambayo huruhusu au huleta adhabu na matokeo yake juu ya kitu, au mtu, au watu kimsingi ni kwa sababu ya utovu wa haki. Laana ni kuonekana kwa upendo mtakatifu na haki ya Mungu. Zaweza kutolewa moja kwa moja na Mungu au kutamkwa na mtumishi Wake mwenye mamlaka. Wakati mwingine, sababu kamilifu za laana hujulikana tu kwa Mungu. Kwa nyongeza, hali ya laana huwatokea wale ambao kwa makusudi hawamtii Mungu na hivyo kujiengua wao wenyewe kutoka kwa Roho wa Bwana.

Bwana aweza kuiondoa laana kwa sababu ya imani ya mtu mmoja au ya watu katika Yesu Kristo na utiifu wao katika sheria na ibada za injili (Alma 23:16–18; 3 Ne. 2:14–16; M ya I 1:3).

Kutumia lugha chafu

Kulaani pia na kutumia lugha ambayo ni chafu, ya kukufuru, au ya dharau.