Viumbe waliobadilishwa Watu waliobadilishwa ili wao wasionje maumivu au mauti hadi ufufuko wao katika mwili usiokufa. Henoko akaenda pamoja na Mungu; naye akatoweka; maana Mungu alimtwaa, Mwa. 5:24 (Ebr. 11:5; M&M 107:48–49). Hakuna mtu ajuaye juu ya kaburi la Musa hata leo, Kum. 34:5–6 (Alma 45:19). Eliya alipanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, 2 Fal. 2:11. Kama ninataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje, Yn. 21:22–23 (M&M 7:1–3). Hutaonja mauti kamwe, 3 Ne. 28:7. Ili wasipate kuonja mauti kulikuwa na mabadiliko yaliyofanyika juu ya miili yao, 3 Ne. 28:38 (4 Ne. 1:14; Morm. 8:10–11). Yohana Kipenzi ataishi hadi Bwana atakapokuja, M&M 7. Nimeichukua Sayuni ya Henoko kifuani pangu mwenyewe, M&M 38:4 (Musa 7:21, 31, 69). Henoko na nduguze ndiyo mji uliohifadhiwa hadi siku ya haki, M&M 45:11–12. Eliya alitwaliwa mbinguni pasipo kuonja mauti, M&M 110:13. Roho Mtakatifu alishuka juu ya wengi, nao wakanyakuliwa katika Sayuni, Musa 7:27.