Misaada ya Kujifunza
Makala ya Imani


Makala ya Imani

Vipengele vya msingi kumi na vitatu vya imani ambavyo waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaviamini.

Joseph Smith kwanza aliviandika katika barua aliyomwandikia John Wentworth, mhariri wa gazeti la Chicago Democrat, katika kujibu maombi yake ya kutaka kujua nini wanachama wa Kanisa wanaamini. Barua hiyo ilikuja kujulikana kama Barua ya Wentworth na kwanza ilichapishwa katika gazeti la Times and Seasons mnamo Machi 1842. Mnamo 10 Oktoba 1880, Makala ya Imani yalikubalika rasmi kama maandiko matakatifu kwa kura ya waumini wa Kanisa na yakajumuishwa kama sehemu ya Lulu ya Thamani Kuu.