Sengenya Ona pia Kusema uovu; Uvumi Kutoa siri za mtu au taarifa juu ya mtu mwingine pasipo idhini ya mtu huyo. Kila neno lisilofaa ambalo mtu atalisema, atajibu juu yake, Mt. 12:36. Watakatifu wanaonywa wasiwe wafitini na wadaku, wakizungumza mambo ambayo hawapaswi kuzungumza, 1 Tim. 5:11–14. Usimseme mabaya jirani yako, M&M 42:27. Waimarishe ndugu zako katika mazungumzo yako yote, M&M 108:7.