Siku za Mwisho Ona pia Ishara za Nyakati; Ujio wa Pili wa Yesu Kristo Wakati ambao sasa tunaishi. Siku (au kipindi cha wakati) ambazo ni mara kabla ya Ujio wa Pili wa Bwana. Niwaambie yatakayowapata siku za mwisho, Mwa. 49:1. Siku ya mwisho Mkombozi atasimama juu ya dunia, Ayu. 19:25. Katika siku za mwisho, nyumba ya Bwana itawekwa imara, Isa. 2:2. Katika siku za mwisho kutakuja nyakati za hatari, 2 Tim. 3:1–7. Wadhihaki wa siku ya mwisho watakana Ujio wa Pili, 2 Pet. 3:3–7. Ninatoa unabii kwenu ninyi kuhusu siku za mwisho, 2 Ne. 26:14–30. Hivyo ndivyo kanisa langu litakavyoitwa katika siku za mwisho, hata Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, M&M 115:4. Kristo atakuja katika siku za mwisho, Musa 7:60.