Yakobo, Kaka wa Bwana
Katika Agano Jipya, ni kaka wa Bwana (Gal. 1:19) na wa Yusufu, Simoni, Juda, na dada kadhaa (Mt. 13:55–56; Mk. 6:3; Yuda 1:1). Pia alijulikana kama Yakobo mwenye Haki na alikuwa na nafasi muhimu katika Kanisa katika Yerusalemu (Mdo. 12:17; 15:13; 1 Kor. 15:7; Gal. 2:9–12). Huenda yeye ndiye aliyeandika waraka wa Yakobo.
Waraka wa Yakobo
Kitabu katika Agano Jipya. Mwanzoni hii ilikuwa ni barua iliyoandikwa kwa makabila kumi na mawili ya Israeli yaliyotawanyika sehemu mbalimbali na huenda kuwa iliandikwa kutoka Yerusalemu. Waraka una mambo yaliyoelezwa wazi juu ya matendo ya dini, ikijumuisha ushauri muhimu katika mlango wa 1 kwamba kama mtu akipungukiwa na hekima, aombe msaada kwa Mungu (Yak. [Bib.] 1:5–6; JS—H 1:9–20). Mlango wa 2 unajishughulisha na imani na matendo. Mlango wa 3–4 inazungumzia juu ya umuhimu wa kuudhibiti ulimi na anawashauri watakatifu wasisemeane mabaya. Mlango wa 5 unawatia moyo Watakatifu kuwa na subira na kuwaita wazee kwa ajili ya kuwabariki wawapo wagonjwa; pia inafundisha juu ya baraka za kusaidia kuwaongoa wengine.