Kuweza kufanya jambo fulani. Kuwa na uwezo juu ya mtu fulani au kitu fulani ni kuweza kudhibiti au kumwamuru mtu huyo au jambo hilo. Katika maandiko, uwezo daima unaunganishwa na nguvu za Mungu au nguvu za mbingu. Mara kwa mara huhusishwa kwa karibu na mamlaka ya ukuhani, ambayo ni ruhusa au haki ya kutenda jambo kwa niaba ya Mungu.
Kwa sababu hii nilikusimamisha wewe, ili kuonyesha katika wewe uwezo wangu, Ku. 9:16 .
Mungu ndiye nguvu na uwezo wangu, 2Â Sam. 22:33 .
Usiwanyime watu mema ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda, Mit. 3:27 .
Mimi hakika nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana, Mika 3:8 .
Nimepewa uwezo wote mbinguni na duniani, Mt. 28:18 .
Wakashangaa mno kwa mafundisho yake: kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo, Lk. 4:32 .
Kaeni humu mjini, hadi mvikwe uwezo utokao juu, Lk. 24:49 .
Kadiri wengi walivyompokea, aliwapa uwezo wa kuwa wana wa Mungu, Yn. 1:12 (M&M 11:30 ).
Mtapokea nguvu, baada ya kujiwa na Roho Mtakatifu, Mdo. 1:8 .
Hakuna nguvu isipokuwa imetoka kwa Mungu, Rum. 13:1 .
Mnalindwa kwa nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu, 1 Pet. 1:3–5 .
Ingawa mwanadamu aweza kuwa na nguvu za kufanya kazi kubwa, kama akijidai katika nguvu zake mwenyewe lazima ataanguka, M&M 3:4 .
Nguvu za kufanya mema ziko ndani ya kila mtu, M&M 58:27–28 .
Katika ibada zifanywazo kwa Ukuhani wa Melkizedeki nguvu za uchamungu hujidhihirisha, M&M 84:19–22 .
Haki za ukuhani zimeungana na hazitenganishwi na nguvu za mbinguni, M&M 121:34–46 .