Huisha Ona pia Ufufuko Kufanya kuwa hai, kufufua, au kumbadilisha mtu ili aweze kuwa katika uwepo wa Mungu. Mungu alituhuisha pamoja na Kristo, Efe. 2:4–5 (Kol. 2:6, 12–13). Kristo aliuawa katika mwili, bali alihuishwa na Roho, 1 Pet. 3:18 (M&M 138:7). Hakuna mtu aliyemwona Mungu, isipokuwa alihuishwa na Roho, M&M 67:11. Ukombozi ni kupitia kwake yeye ambaye huhuisha vitu vyote, M&M 88:16–17. Watakatifu watahuishwa na kutwaliwa kumlaki Kristo, M&M 88:96. Adamu alihuishwa katika utu wa ndani, Musa 6:65.