Mosia, Baba wa Benjamini Ona pia Benjamini, Baba wa Mosia; Zarahemla Katika Kitabu cha Mormoni, ni nabii wa Wanefi aliyefanywa kuwa mfalme juu ya watu wa Zarahemla. Mosia alionywa aikimbie nchi ya Nefi, Omni 1:12. Akawavumbua watu wa Zarahemla, Omni 1:14–15. Alifanya watu wa Zarahemla wafundishwe katika lugha yake, Omni 1:18. Aliteuliwa kuwa mfalme wa watu wa muungano, Omni 1:19. Mwanawe, Benjamini, alitawala baada ya kifo chake, Omni 1:23.