Jaribu, Majaribu Ona pia Haki ya uamuzi; Ibilisi; Stahimili Pima uwezo wa mtu wa kuchagua mema badala ya maovu; kishawishi cha kutenda dhambi na kumfuata Shetani badala ya Mungu. Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na ovu, Mt. 6:13 (3 Ne. 13:12). Mungu hatawaacha mjaribiwe kupita mwezayo kuvumilia, 1 Kor. 10:13. Kristo alijaribiwa kama sisi, Ebr. 4:14–15. Heri mtu yule mwenye kustahmili majaribu, Yak. (Bib.) 1:12–14. Majaribu ya adui hayawezi kuwalemea wale wanaosikiliza neno la Mungu, 1 Ne. 15:24 (Hel. 5:12). Mwanadamu hangeweza kujichagulia mwenyewe isipokuwa alishawishiwa na kimoja au kingine, 2 Ne. 2:11–16. Kesheni na kusali daima, ili msipate kujaribiwa kupita lile mnaloweza kuvumilia, Alma 13:28. Wafundisheni kuhimili kila jaribu la ibilisi, kwa imani yao juu ya Bwana Yesu Kristo, Alma 37:33. Salini daima msije mkaingia majaribu, 3 Ne. 18:15, 18 (M&M 20:33; 31:12; 61:39). Jihadhari na kiburi, usije ukaingia majaribuni, M&M 23:1. Adamu akawa chini ya mapenzi ya ibilisi kwa sababu alikubali majaribu, M&M 29:39–40. Niliachwa katika namna zote za majaribu, JS—H 1:28.