Maongozi ya Mungu, Shawishi Ona pia Roho Mtakatifu; Ufunuo Mwongozo mtakatifu utolewao na Mungu kwa mwanadamu. Maongozi mara kwa mara huja mawazoni au moyoni mwa mtu katika njia tofauti ya kiroho. Baada ya moto ikaja sauti ndogo tulivu, 1 Fal. 19:12. Roho Mtakatifu atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha mambo yote, Yn. 14:26. Roho wa kweli atawaongoza katika kweli yote, Yn. 16:13. Niliongozwa na Roho, bila ya kufahamu mapema mambo ambayo nitayafanya, 1 Ne. 4:6. Sauti ya Bwana ikanijia mawazoni mwangu, Eno. 1:10. Kila kitu chenye kukaribisha na kushawishi kutenda mema kimeongozwa na Mungu, Moro. 7:13–16. Sikusema amani akilini mwako, M&M 6:23. Nitakuambia mawazoni mwako na moyoni mwako, M&M 8:2. Roho wangu atayaangaza mawazo yako, ambayo yataijaza nafsi yako kwa shangwe, M&M 11:13. Utapewa katika saa ile kile utakachozungumza au kuandika, M&M 24:6 (M&M 84:85). Sauti ndogo tulivu hunongʼona na kupenya vitu vyote, M&M 85:6.