Abinadi Ona pia Kifo cha kishahidi, Mfiadini Nabii wa Kinefi katika Kitabu cha Mormoni. Alitoa unabii kwamba Mungu angewaadhibu watu wa mfalme mwovu Nuhu isipokuwa kama watatubu, Mos. 11:20–25. Alitiwa gerezani kwa kutoa unabii wa angamizo la Mfalme Nuhu na watu wake, Mos. 12:1–17. Aliwafundisha makuhani waovu wa Mfalme Nuhu juu ya sheria ya Musa na juu ya Kristo, Mos. 12–16. Alma Mkubwa aliamini na kuandika maneno yake, Mos. 17:2–4. Aliunguzwa kwa moto hadi kufa na Mfalme Nuhu, Mos. 17:20.