Isakari
Mwana wa Yakobo na Lea katika Agano la Kale (Mwa. 30:17–18; 35:23; 46:13). Wazao wake walikuja kuwa moja ya makabila kumi na mawili ya Israeli.
Kabila la Isakari
Baraka za Yakobo kwa Isakari zinapatikana katika Mwanzo 49:14–15. Baada ya kufanya makazi Kaanani, kabila hili lilipata baadhi sehemu ya nchi iliyo kuwa tajiri sana katika Palestina ikiwa pamoja na nyanda za Esdraloni. Ndani ya mipaka ya Isakari kulikuwa na sehemu kadhaa muhimu katika historia ya Uyahudi, kwa mfano, Karmeli, Megido, Dothani, Gilboa, Yezereeli, Taboa, na Nazarethi (Yos. 19:17–23).