Njia ambayo kwayo mwanadamu akawa na mwili wenye kufa hapa duniani. Wakati Adamu na Hawa walipokula tunda lililokatazwa, wakawa wenye mwili wenye kufa, ambako, ni kujiweka chini ya dhambi na mauti. Adamu akawa “mwenye mwili” wa kwanza juu ya dunia (Musa 3:7). Ufunuo wa siku za mwisho unaweka wazi kwamba Anguko ni baraka na kwamba Adamu na Hawa yapaswa waheshimiwe kama wazazi wa kwanza wa wanadamu wote.
Anguko lilikuwa ni hatua muhimu katika makuzi ya mwanadamu. Kwa sababu Mungu alijua kwamba Anguko lingetokea, alipanga katika maisha kabla ya kuzaliwa kuwepo kwa Mwokozi. Yesu Kristo alikuja wakati wa meridiani ili kulipia kosa la Anguko la Adamu na pia kwa ajili ya dhambi za mtu binafsi kwa sharti la toba ya mtu.