Imba Ona pia Muziki; Wimbo Kuabudu na kumsifu Mungu katika wimbo na beti za muziki. Mwimbieni Bwana, 1 Nya. 16:23–36 (Zab. 96). Mwimbieni Bwana, na mpeni shukrani, Zab. 30:4. Mfanyieni Bwana sauti za furaha, Zab. 100:1. Walipokuwa wamekwisha kuimba wimbo wa Kanisa, walitoka kwenda katika mlima wa Mizeituni, Mt. 26:30. Roho Mtakatifu aliwaongoza kuimba, Moro. 6:9. Wimbo wa mwenye haki ni sala kwangu, M&M 25:12. Kama mmefurahi, msifuni Bwana kwa kuimba, M&M 136:28.