Uchaji Ona pia Heshima; Hofu Heshima kubwa kwa vitu vitakatifu; staajabika. Bwana alimwamuru Musa kuvua viatu vyake, kwa kuwa alisimama juu ya ardhi takatifu, Ku. 3:4–5. Mungu huogopwa na ni wa kuhofiwa, Zab. 89:7. Tumtumikie Mungu kwa kumpendeza na kwa kuonyesha unyenyekevu na hofu ya kimungu, Ebr. 12:28. Moroni akajiinamisha chini, na akasali kwa nguvu sana, Alma 46:13. Umati ulianguka chini na wakamwabudu Kristo, 3 Ne. 11:12–19. Inama mbele zangu, M&M 5:24. Vitu vyote husujudu kwa upole na unyenyekevu mbele za kiti cha enzi cha Mungu, M&M 76:93. Akili zenu zilikuwa zimetiwa giza kwa sababu mmeyachukua bila uzito mambo mliyoyapokea, M&M 84:54–57. Kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri, M&M 88:104. Kwa heshima au kwa kuonyesha unyenyekevu kwa jina la Kiumbe Mkuu, Kanisa likauita ukuhani huo Melkizedeki, M&M 107:4. Baraka zitamwagwa juu ya wale wenye kuonyesha unyenyekevu kwa Bwana katika nyumba yake, M&M 109:21.