Misaada ya Kujifunza
Elia


Elia

Kuna matumizi kadha wa kadha ya jina hili au cheo cha Elia katika Maandiko:

Eliya

Elia ni mtindo wa Agano Jipya (Kiyunani) ya Eliya (Kiebrania), kama katika Mt. 17:3–4, Lk. 4:25–26, na Yak. (Bib.) 5:17. Katika matukio haya, Elia alikuwa ndiye nabii wa kale Eliya ambaye huduma yake imeandikwa katika Wafalme 1 na 2.

Mtangulizi

Elia pia ni cheo cha mtu aliye mtangulizi. Kwa mfano, Yohana Mbatizaji alikuwa Elia, kwa sababu yeye alitumwa kuitengeneza njia kwa ajili ya Yesu (Mt. 17:12–13).

Mrejeshaji

Cheo cha Elia pia kimetumiwa kwa wengine ambao walikuwa na kazi maalumu ya kutimiza, kama vile Yohana Mfunuzi (M&M 77:14) na Gabrieli (Lk. 1:11–20; M&M 27:6–7; 110:12).

Mtu aliyekuwa katika kipindi cha Ibrahimu

Nabii aliyeitwa Esaiya au Elia ambaye ni dhahiri aliishi katika siku za Ibrahimu (M&M 84:11–13; 110:12).