Ndimi, Kipawa cha Ona Ulimi; Vipawa vya Roho Kipawa cha Roho Mtakatifu ambacho huwaruhusu watu walio na mwongozo wa kiuungu kunena katika, au kuelewa, au kutafsiri lugha ngeni. Tunaamini katika kipawa cha ndimi (M ya I 1:7). Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, na wakaanza kunena kwa ndimi zingine, Mdo. 2:4. Mtu anenaye katika ndimi isiyojulikana hasemi na wanadamu, bali na Mungu, 1 Kor. 14:1–5, 27–28. Ndimi ni ishara kwao wale wasioamini, 1 Kor. 14:22–28. Kisha waja ubatizo wa moto na wa Roho Mtakatifu; na ndipo mtakaponena kwa ndimi za malaika, 2 Ne. 31:13–14. Amaleki aliwasihi watu wote kuamini katika kunena kwa ndimi, Omni 1:25. Imetolewa kwa wengine kunena kwa ndimi; na mwingine kutafsiri ndimi, M&M 46:24–25 (1 Kor. 12:10; Moro. 10:8, 15–16). Na kipawa cha ndimi kimwagwe, M&M 109:36.