Moroni, Kapteni Ona pia Bendera ya Uhuru Katika Kitabu cha Mormoni, ni kamanda mwaminifu wa jeshi la Wanefi aliyeishi takribani miaka 100 K.K. Moroni aliteuliwa kuwa kapteni mkuu wa majeshi yote ya Wanefi, Alma 43:16–17. Aliwatia moyo askari wa Wanefi kupigana kwa ajili ya uhuru wao, Alma 43:48–50. Alitengeneza bendera ya uhuru kutokana na kipande cha koti lake, Alma 46:12–13. Alikuwa mtu wa Mungu, Alma 48:11–18. Alikasirishwa na serikali kwa sababu ya tofauti zao juu ya uhuru wa nchi, Alma 59:13.