Nyoka wa shaba nyeupe
Nyoka wa shaba nyeupe aliyetengenezwa na Musa kwa amri ya Mungu ili kuwaponya Waisraeli ambao walikuwa wameumwa na nyoka wakali (nyoka wenye sumu) nyikani (Hes. 21:8–9). Nyoka huyu wa shaba nyeupe alitundikwa kwenye mlingoti na “kuinuliwa juu ili kwamba mtu yeyote ambaye angeliangalia apate kuishi” (Alma 33:19–22). Bwana alielezea kwa kuinuliwa kwa yule nyoka nyikani kama ni ishara yake Yeye mwenyewe akiwa ameinuliwa juu ya msalaba (Yn. 3:14–15). Ufunuo wa siku za mwisho unathibitisha historia juu ya nyoka wakali na jinsi watu walivyokuwa wameponywa (1 Ne. 17:41; 2 Ne. 25:20; Hel. 8:14–15).