Obadia
Nabii wa Agano la kale aliyetabiri maangamizi ya Edomu. Yawezekana alitoa unabii katika wakati wa utawala wa Yehoramu (848–844 K.K.) au wakati wa uvamizi wa Babilonia katika mwaka 586 K.K.
Kitabu cha Obadia
Ni kitabu katika Agano la Kale. Kina mlango mmoja tu. Ndani yake, Obadia aliandika kuanguka kwa Edomu na alitoa unabii kwamba waokozi watakwea juu ya Mlima Sayuni.