Utukufu Ona pia Madaraja ya Utukufu; Nuru, Nuru ya Kristo; Ukweli Katika maandiko, ni utukufu mara kwa mara umetajwa kuwa ni nuru na ukweli wa Mungu. Pia waweza kutajwa kuwa ni sifa au heshima na hali fulani ya uzima wa milele au ya utukufu wa Mungu. Mtakatifu ni Bwana wa majeshi: dunia yote imejaa utukufu wake, Isa. 6:3 (2 Ne. 16:3). Tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, 2 Kor. 3:18. Ataniinua juu ili niishi pamoja naye katika utukufu, Alma 36:28. Tukufu tutakazopokelewa katika ufufuko zitatofautiana kulingana na haki, M&M 76:50–119. Utukufu wa Mungu ni akili, M&M 93:36. Utukufu wa Mungu ni kutokufa maisha na uzima wa milele wa mwanadamu, Musa 1:39. Niliwaona Watu wawili, ambao uangavu na utukufu wao wapita maelezo yote, JS—H 1:17.