Agano la Ibrahimu
Ibrahimu aliipokea injili na akatawazwa katika ukuhani wa juu (M&M 84:14; Ibr. 2:11), naye akaingia katika ndoa ya selestia, ambayo ni agano la kuinuliwa (M&M 131:1–4; 132:19, 29). Ibrahimu alipokea ahadi ya kwamba baraka zote za maagano haya zitatolewa kwa wazao wake watakaozaliwa duniani (M&M 132:29–31; Ibr. 2:6–11). Kwa pamoja, maagano na ahadi hizi ndiyo huitwa agano la Ibrahimu. Urejesho wa agano hili ulikuwa ndiyo Urejesho wa injili katika siku za mwisho, kwani kwa hiyo mataifa yote ya dunia yamebarikiwa (Gal. 3:8–9, 29; M&M 110:12; 124:58; Ibr. 2:10–11).