Hekalu la Kirtland, Ohio (Marekani)
Hekalu la kwanza lililojengwa na kanisa katika nyakati za sasa. Watakatifu walilijenga huko Kirtland, kulingana na amri ya Bwana (M&M 94:3–9). Dhumuni mojawapo lilikuwa ni kupata mahali ambapo waumini wa Kanisa wanaostahili waweze kupokea nguvu za kiroho, mamlaka, na maarifa (M&M 109–110). Liliwekwa wakfu, mnamo 27 Machi 1836; sala ya kuweka wakfu ilitolewa na Joseph Smith Nabii kwa ufunuo (M&M 109). Bwana alitoa mafunuo kadhaa yaliyo muhimu na kurejesha funguo za ukuhani zilizohitajika katika hekalu hili (M&M 110; 137). Halikutumiwa kwa ibada kamilifu za hekalu kama zinavyotolewa katika mahekalu siku hizi.