Mtoto, Watoto Ona pia Baraka, Bariki, Barikiwa—Baraka za watoto; Familia; Kuwajibika, Uwajibikaji, Wajibika; Lipia dhambi, Upatanisho; Ubatizo wa Watoto Wachanga; Wokovu—Wokovu wa watoto Mtu aliye mdogo, ambaye bado hajafikia balehe. Akina baba na akina mama wawafundishe watoto wao kutii mapenzi ya Mungu. Watoto hawana dhambi hadi wafikiapo umri wa uwajibikaji (Moro. 8:22; M&M 68:27). Watoto ndiyo urithi kutoka kwa Bwana, Zab. 127:3–5. Mlee mtoto katika njia impasayo, Mit. 22:6. Waacheni watoto wadogo waje kwangu na msiwazuie, Mt. 19:14. Watiini wazazi wenu, Efe. 6:1–3 (Kol. 3:20). Pasipo Anguko, Adamu na Hawa wasingelikuwa na watoto, 2 Ne. 2:22–23. Wafundisheni watoto kutembea katika ukweli na katika kiasi, Mos. 4:14–15. Watoto wadogo wanao uzima wa milele, Mos. 15:25. Yesu akawachukua watoto wadogo na kuwabariki, 3 Ne. 17:21. Na watoto wako wote wafundishwe juu ya Bwana, na amani ya watoto wako itakuwa kubwa, 3 Ne. 22:13 (Isa. 54:13). Watoto wadogo hawahitaji toba au ubatizo, Moro. 8:8–24. Watoto wadogo wamekombolewa tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu kwa njia ya Mwanangu wa Pekee, M&M 29:46–47. Wazazi yawapasa wawafundishe watoto wao kanuni za injili na desturi zake, M&M 68:25, 27–28. Watoto ni watakatifu kwa njia ya upatanisho wa Kristo, M&M 74:7. Wazazi wanaamriwa kuwalea watoto wao katika nuru na kweli, M&M 93:40. Watoto wanao kufa kabla ya umri wa uwajibikaji wanaokolewa katika ufalme wa selestia, M&M 137:10.