Mchungaji Mwema Ona pia Yesu Kristo Yesu Kristo ndiye Mchungaji Mwema. Kimfano, wafuasi wake ni kama kondoo ambao Yesu anawachunga. Bwana ndiye mchungaji wangu, Zab. 23:1. Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Isa. 40:11. Ndivyo nitakavyo watafuta kondoo wangu, Eze. 34:12. Mimi ndiye mchungaji mwema, Yn. 10:14–15. Yesu ndiye yule mchungaji mkuu wa kondoo, Ebr. 13:20. Huwahesabu kondoo wake nao humjua yeye, 1 Ne. 22:25. Mchungaji mwema huwaita ninyi katika jina lake, ambalo ni Kristo, Alma 5:38, 60. Kutakuwako na kundi moja, na mchungaji mmoja, 3 Ne. 15:21 (Yn. 10:16).