Katiba Ona pia Sheria; Utawala Katika kitabu cha Mafundisho na Maagano, “Katiba” inamaanisha Katiba ya Muungano wa Mataifa ya Marekani, ambayo iliandikwa kwa mwongozo wa kiungu ili kutengeneza njia kwa ajili ya urejesho wa injili. Sheria ya kikatiba haina budi kuungwa mkono, M&M 98:5–6. Bwana ndiye aliyesababisha katiba hii iwekwe, M&M 101:77, 80.