Kuinuliwa Ona pia Lipia dhambi, Upatanisho; Mwanadamu, Wanadamu—Mwanadamu, uwezekano wa kuwa kama Baba wa Mbinguni; Taji; Utukufu wa Selestia; Uzima wa Milele Hali ya furaha iliyo ya juu zaidi na utukufu katika ufalme wa selestia. Katika uwepo wako ziko utimilifu wa shangwe, Zab. 16:11. Wao ndiyo miungu, hata wana wa Mungu—kwa hiyo, vitu vyote ni vyao, M&M 76:58–59. Watakatifu watapata urithi wao na watafanywa kuwa sawa naye, M&M 88:107. Malaika hawa hawakuishi kulingana na sheria zangu; kwa hiyo, watabaki wametengana mmoja mmoja, pasipo kuinuliwa, M&M 132:17. Wanaume na wanawake lazima waoe na kuoana kulingana na sheria ya Mungu ili kupata kuinuliwa, M&M 132:19–20. Mlango ni mwembamba na njia imesonga iongozayo katika kuinuliwa, M&M 132:22–23. Ibrahimu, Isaka, na Yakobo wameingia ndani ya kuinuliwa kwao, M&M 132:29, 37. Ninafunga juu yako kuinuliwa kwao, M&M 132:49.