Makerubi Maumbo yanayowakilisha viumbe wa mbinguni, umbile lenyewe halisi likiwa halijulikani. Makerubi waliitwa ili kulinda maeneo matakatifu. Bwana akaweka makerubi kuilinda njia ya mti wa uzima, Mwa. 3:24 (Alma 12:21–29; 42:2–3; Musa 4:31). Sanamu ziwakilishazo makerubi ziliwekwa juu ya kiti cha rehema, Ku. 25:18, 22 (1 Fal. 6:23–28; Ebr. 9:5). Makerubi wametajwa katika maono ya Ezekieli, Eze. 10; 11:22.