Tukuza Ona pia Heshima; Uchaji Kumchukulia mtu fulani au kitu fulani kama chenye kustahili na chenye thamani, hususani katika mtazamo wa kiinjili. Alidharauliwa, na hatukumhesabu kuwa kitu, Isa. 53:3–4. Lile ambalo linatukuzwa miongoni mwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu, Lk. 16:15. Kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake, Flp. 2:3. Bwana huhesabu wenye mwili wote kuwa kitu kimoja, 1 Ne. 17:35. Kila mwanadamu yapasa amheshimu jirani yake kama yeye mwenyewe, Mos. 27:4 (M&M 38:24–25). Katika siku ya amani yao waliuchukulia kwa wepesi ushauri wangu, M&M 101:8.