Amua, Hukumu Ona pia Hukumu ya mwisho; Shutuma, Shutumu; Yesu Kristo—Mwamuzi Kupima tabia kwa kuilinganisha na kanuni za injili; kuamua; kutambua mema na maovu. Musa aliketi ili awahukumu watu, Ku. 18:13. Kwa haki utamhukumu jirani yako, Law. 19:15. Msihukumu, nanyi msije mkahukumiwa, Mt. 7:1 (TJS, Mt. 7:1–2; Lk. 6:37; 3 Ne. 14:1). Kadiri wengi walivyotenda dhambi katika sheria, watahukumiwa kwa sheria, Rum. 2:12. Watakatifu watauhukumu ulimwengu, 1 Kor. 6:2–3. Mwana wa Mungu asiye na mwisho alihukumiwa na ulimwengu, 1 Ne. 11:32. Mitume Kumi na Wawili wa Mwanakondoo watayahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli, 1 Ne. 12:9 (M&M 29:12). Mauti, jehanamu, ibilisi, na wale wote walioshikiliwa hao lazima watahukumiwa, 2 Ne. 28:23 (1 Ne. 15:33). Kama utamhukumu mtu akuombaye msaada wa kitu, laana yako itakuwa nyingi kiasi gani kwa kumnyima hicho kitu chako, Mos. 4:22. Wanadamu watahukumiwa kulingana na matendo yao, Alma 41:3. Hukumu kwa haki, nawe utarejeshewa haki tena, Alma 41:14. Ulimwengu utahukumiwa na vitabu vitakavyoandikwa, 3 Ne. 27:23–26 (Ufu. 20:12). Mabaki la watu hawa watahukumiwa na wale kumi na wawili ambao Yesu aliwachagua katika nchi hii, Morm. 3:18–20. Mormoni alielezea jinsi ya kuhukumu kati ya mema na maovu, Moro. 7:14–18. Weka imani yako katika yule Roho aongozaye katika kuhukumu kwa haki, M&M 11:12. Mnapaswa kusema mioyoni mwenu—Mungu na ahukumu kati yangu mimi na wewe, M&M 64:11. Kanisa la Bwana litayahukumu mataifa, M&M 64:37–38. Mwana alizitembelea roho zilizokuwa kifungoni ili zipate kuhukumiwa kulingana na mwanadamu katika mwili, M&M 76:73 (1 Pet. 4:6). Askofu atakuwa mwamuzi wa wote, M&M 107:72–74. Bwana atawahukumu watu wote kulingana na matendo yao, kulingana na tamaa za mioyo yao, M&M 137:9.