Masiya
Aina ya neno la Kiaramai na Kiebrania lenye maana ya “mpakwa mafuta.” Katika Agano Jipya Yesu anaitwa Kristo, ambalo ni la Kiyunani lililo sawa na Masiya. Maana yake Nabii mpakwa mafuta, Kuhani, Mfalme na Mkombozi ambaye kuja kwake Wayahudi walikutarajia kwa hamu kubwa.
Wayahudi wengi walitazamia tu mkombozi kutoka mamlaka ya Kirumi na kwa ustawi mkubwa zaidi wa kitaifa; hivyo basi, wakati Masiya alipokuja, viongozi na watu wengine wengi Walimkataa. Wale waliokuwa wanyenyekevu na waaminifu tu, waliweza kuona ndani ya Yesu wa Nazarethi Kristo wa kweli (Isa. 53; Mt. 16:16; Yn. 4:25–26).