Kutokuwa Adilifu, Siyo Adilifu Ona pia Chafu, Uchafu; Dhambi; Haki, Uadilifu, enye Uadilifu; Ovu, Uovu; Sio mcha mungu Ovu, sio haki; watu ambao hawampendi Mungu au mambo ya Mungu na ambao hawaungi mkono kazi Yake. Wadhalimu hawatarithi ufalme wa Mungu, 1 Kor. 6:9–10. Wale ambao hufurahia katika udhalimu watahukumiwa, 2 The. 2:12. Yesu Kristo anaweza kutusafisha kutokana na udhalimu wote, 1 Yoh. 1:9. Mfalme dhalimu huzichafua njia zote za haki, Mos. 29:23. Msingi wa angamizi unawekwa na udhalimu wa wanasheria na waamuzi, Alma 10:27. Ninawatuma ninyi kuwakemea walimwengu juu ya matendo yao ya udhalimu, M&M 84:87. Nafsi lazima itakaswe kutokana na udhalimu wote, M&M 88:17–18. Tabia ya karibu wanadamu wote ni kuanza kutumia utawala pasipo haki, M&M 121:39.