Utakaso Ona pia Hesabu kwa haki, Kuhesabiwa haki; Lipia dhambi, Upatanisho; Yesu Kristo Njia ya kuwa huru na dhambi, sio na doa, safi, na takatifu kwa njia ya upatanisho wa Yesu Kristo (Musa 6:59–60). Mungu amewachagua mpate wokovu kwa njia ya utakaso na Roho, 2 The. 2:13. Tumetakaswa kwa njia ya kutolewa kwa mwili wa Yesu, Ebr. 10:10. Yesu aliteseka ili apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, Ebr. 13:12. Makuhani wakuu walitakaswa na mavazi yao yakaoshwa kuwa meupe kwa njia ya damu ya Mwanakondoo, Alma 13:10–12. Utakaso ambao huja kwa wale ambao huiachia mioyo yao kwa Mungu, Hel. 3:33–35. Tubuni ili mpate kutakaswa kwa kumpokea Roho Mtakatifu, 3 Ne. 27:20. Utakaso kupitia neema ya Yesu Kristo ni haki na kweli, M&M 20:31. Yesu alikuja kuutakasa ulimwengu, M&M 76:41. Jitakaseni ninyi wenyewe ili mawazo yenu yawe tu kwa Bwana, M&M 88:68.