Misaada ya Kujifunza
Ufufuko


Ufufuko

Kuungana tena kwa mwili wa kiroho pamoja na mwili wa kawaida wa nyama na mifupa baada ya kifo. Baada ya ufufuko, roho na mwili kamwe havitatengana tena, na mtu atakuwa mtu asiyekufa. Kila mtu aliyezaliwa duniani atafufuka kwa sababu Yesu alishinda mauti (1 Kor. 15:20–22).

Yesu Kristo alikuwa mtu wa kwanza kufufuka katika dunia hii (Mdo. 26:23; Kol. 1:18; Ufu. 1:5). Agano Jipya linatoa ushahidi wa kutosha kwamba Yesu alifufuka pamoja na mwili Wake wa kawaida: kaburi Lake lilikuwa wazi, Alikula samaki na asali, Alikuwa na mwili wa nyama na mifupa, watu Walimgusa, na malaika walisema Amefufuka (Mk. 16:1–6; Lk. 24:1–12, 36–43; Yn. 20:1–18). Ufunuo wa siku za mwisho unathibitisha ukweli juu ya Ufufuko wa Kristo na wa wanadamu wote (Alma 11:40–45; 40; 3 Ne. 11:1–17; M&M 76; Musa 7:62).

Watu wote hawatafufuka katika utukufu mmoja (1 Kor. 15:39–42; M&M 76:89–98), wala hawatafufuka kwa wakati mmoja (1 Kor. 15:22–23; Alma 40:8; M&M 76:64–65, 85; 88:96–102). Watakatifu wengi walifufuka baada ya Ufufuko wa Kristo (Mt. 27:52). Waadilifu watafufuka kabla ya waovu nao watatoka katika Ufufuko wa Kwanza (1 The. 4:16); wenye dhambi wasiotubu watatoka katika ufufuko wa mwisho (Ufu. 20:5–13; M&M 76:85).