Mpatanishi Ona pia Lipia dhambi, Upatanisho; Yesu Kristo Mwombezi au msuluhishi. Yesu Kristo ni mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu. Upatanisho Wake ulifanya njia iwezekane kwa watu kutubu dhambi zao na kupatanishwa na Mungu. Hakuna mtu ajaye kwa Baba ila kwa njia ya Yesu Kristo, Yn. 14:6. Kuna mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, 1 Tim. 2:5. Kristo ni mpatanishi wa agano lililo bora, Ebr. 8:6 (Ebr. 9:15; 12:24; M&M 107:19). Masiya Mtakatifu atafanya maombezi kwa watoto wote wa watu, 2 Ne. 2:9 (Isa. 53:12; Mos. 14:12). Mtazameni yule Mpatanishi mkuu, 2 Ne. 2:27–28. Tunafanywa kuwa wakamilifu kupitia Yesu yule mpatanishi wa agano jipya, M&M 76:69.