Lugha chafu Ona pia Kukufuru, Kufuru Utovu wa heshima au dharau kwa mambo matakatifu; hususani, kutoheshimu jina la Mungu. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, Ku. 20:7 (2 Ne. 26:32; Mos. 13:15; M&M 136:21). Kwa nini tunakufuru agano la baba zetu, Mal. 2:10. Kila neno lisilo na maana watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo katika hukumu, Mt. 12:34–37. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana, haifai mambo hayo kuwa hivyo, Yak. (Bib.) 3:10. Maneno yetu yatatuhukumu sisi, Alma 12:14 (Mos. 4:30). Na watu wote wajihadhari namna wanavyolichukua jina langu katika midomo yao, M&M 63:61–62.