Amri za Mungu Ona pia Amri Kumi; Dhambi; Mtiifu, Tii, Utii; Neno la Mungu; Sheria Sheria na matakwa ambayo Mungu huyatoa kwa wanadamu, kwa mtu binafsi au kwa kikundi. Kushika amri za Mungu kutamletea baraka za Bwana na kwa aliye mtiifu (M&M 130:21). Nuhu alifanya kulingana na yale yote ambayo Mungu alimwamuru, Mwa. 6:22. Enendeni katika sheria zangu, na kushika amri zangu, Law. 26:3. Shika amri zangu, na ukaishi, Mit. 4:4 (Mit. 7:2). Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu, Yn. 14:15 (M&M 42:29). Lolote tuombalo, twalipokea kwake, kwa sababu tunazishika amri zake, 1 Yoh. 3:22. Amri zake si nzito, 1 Yoh. 5:3. Uwe imara katika kushika amri, 1 Ne. 2:10. Bwana hatoi amri isipokuwa amewatayarishia njia, 1 Ne. 3:7. Lazima nifanye kulingana na amri kali za Mungu, Yak. (KM) 2:10. Ilimradi mtazishika amri zangu, mtastawi katika nchi, Yar. 1:9 (Alma 9:13; 50:20). Jifunze katika ujana wako kuzishika amri za Mungu, Alma 37:35. Amri hizi ni zangu, M&M 1:24. Zitafuteni amri hizi, M&M 1:37. Wale wasiozishika amri hawawezi kuokolewa, M&M 18:46 (M&M 25:15; 56:2). Amri zangu ni za kiroho; siyo za asili au za kimwili, M&M 29:35. Amri hutolewa ili tupate kufahamu mapenzi ya Bwana, M&M 82:8. Sielewi, isipokuwa Bwana ameniamuru, Musa 5:6. Bwana atawapima wanadamu ili kuona kama watafanya yale yote atakayo waamuru, Ibr. 3:25.