Walawi
Kitabu katika Agano la Kale ambacho kinasimulia juu ya kazi za kikuhani katika Israeli. Kinasisitiza utukufu wa Mungu na kanuni ambazo kwazo watu Wake wangeliweza kuishi na kuwa watakatifu. Madhumuni yake ni kufundisha kanuni za tabia njema na kweli za dini za torati ya Musa kwa njia ya ibada. Musa ndiye aliyeandika Kitabu cha Walawi.
Mlango wa 1–7 inaelezea ibada za dhabihu. Mlango wa 8–10 inaelezea ibada iliyofanywa katika kuwaweka wakfu makuhani. Mlango wa 11 unaelezea ni nini kinachoweza au kisichoweza kuliwa na kipi kilicho safi au kisicho safi. Mlango wa 12 unajadili wanawake baada ya kuzaa. Mlango wa 13–15 ni sheria zinazohusu uchafu katika sherehe safi. Mlango wa 16 una ibada inayotakiwa kufanywa katika Siku ya Upatanisho. Mlango wa 17–26 ina mkusanyiko wa kanuni za sheria zinazoshughulikia sherehe za kidini na kijamii. Mlango wa 27 unaelezea kwamba Bwana aliiamuru Israeli kuweka wakfu nafaka zao, kondoo na ngʼombe wao kwa Bwana.