Ushirika Ona pia Umoja; Upendo Kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho, ushirika ni pamoja na kutoa ushirikiano wa kirafiki, kuhudumiana, kuinuana, na kuwaimarisha wengine. Mpende jirani yako kama nafsi yako, Law. 19:18 (Mt. 19:19; M&M 59:6). Utakapoongoka, waimarishe ndugu zako, Lk. 22:32. Mmekuwa wanafunzi wangu mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi, Yn. 13:35. Lisha kondoo wangu, Yn. 21:15–17. Waliomba kwamba tujichukulie juu yetu shirika hili la kuwahudumia Watakatifu, 2 Kor. 8:1–5. Ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwanawe, 1 Yoh. 1:3. Wanefi na Walamani walishirikiana, Hel. 6:3. Na kila mtu ampende ndugu yake kama vile ajipendavyo yeye mwenyeye, M&M 38:24–25. Kama ninyi si wamoja, si wangu, M&M 38:27. Ninakupokea katika shirika kuwa rafiki yako na ndugu yako, M&M 88:133.