Misaada ya Kujifunza
Yoeli


Yoeli

Nabii katika nchi ya Yuda katika Agano la Kale. Siku za maisha yake hazina uhakika—yawezekana kuwa aliishi katikati ya wakati wa utawala wa Yoashi, kabla ya mwaka 850 K.K. na kurudi kwa kabila la Yuda kutoka utumwani Babeli.

Kitabu cha Yoeli

Kitabu hiki kinaelezea juu ya unabii uliotolewa na Yoeli baada ya nchi ya Yuda kuwa imepigwa kwa ukame mkali na nzige (Yoe. 1:4–20). Yoeli aliwahakikishia watu kuwa kupitia toba wangeliweza tena kupokea baraka za Mungu (Yoe. 2:12–14).

Mlango wa 1 ni wito kwa ajili ya kusanyiko la kiroho katika nyumba ya Bwana. Mlango wa 2 unasimulia juu ya vita na ukiwa utakaoitangulia Milenia. Mlango wa 3 unazungumzia juu ya siku za mwisho na inatamka kwa dhati kwamba mataifa yote yatakuwa katika vita lakini mwishowe Bwana atakaa katika Sayuni.

Petro alinukuu unabii wa Yoeli wa kumwagwa kwa roho katika siku ile ya Pentekoste (Yoe. 2:28–32; Mdo. 2:16–21). Malaika Moroni pia alinukuu mistari hii hii kwa Joseph Smith. (JS—H 1:41).