Kalebu
Mmoja wa wale waliotumwa na Musa kuchunguza nchi ya Kanaani katika mwaka wa pili baada ya Kutoka. Yeye na Yoshua pekee yao walirudisha taarifa ya kweli juu ya nchi (Hes. 13:6, 30; 14:6–38). Wao pekee yao kati ya wale wote waliondoka Misri walisalia katika ile miaka arobaini ya nyikani (Hes. 26:65; 32:12; Kum. 1:36) na kuingia Kanaani (Yos. 14:6–14; 15:13–19).