Shida Ona pia Jaribu, Majaribu; Mateso, Tesa; Rudi, Kurudiwa; Stahimili Kupitia shida—majaribu, dhiki, na huzuni—mwanadamu aweza kupata matatizo mengi ambayo humpeleka katika makuzi ya kiroho na makuzi ya milele kwa kumgeukia Bwana. Mungu mwenyewe ndiye aliyewaokoa ninyi katika shida zenu zote na taabu zenu, 1 Sam. 10:19. Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Zab. 107:6, 13, 19, 28. Ingawa Bwana atawapeni chakula cha shida, lakini walimu wako hawataondolewa, Isa. 30:20–21. Kwani lazima kuwe na upinzani katika mambo yote, 2 Ne. 2:11. Kama kamwe hawakuonja machungu, wasingeliweza kuyajua matamu, M&M 29:39. Shida zako zitakuwa kwa muda mfupi tu, M&M 121:7–8. Mambo haya yote yatakupa wewe uzoefu, nayo yatakuwa kwa faida yako, M&M 122:5–8. Wanaonja machungu, ili wapate kujua kutuza chema, Musa 6:55.