Moto Ona pia Batiza, Ubatizo; Dunia—Kutakaswa kwa dunia; Jehanamu; Roho Mtakatifu Ishara ya kuoshwa, kusafishwa, au kutakaswa. Moto waweza pia kutumika kama ishara ya uwepo wa Mungu. Mungu wenu ni moto ulao, Kum. 4:24. Bwana huwafanya watumishi wake kuwa moto wa miali, Zab. 104:4. Bwana wa majeshi atawajilia kwa miale ya moto uteketezao, Isa. 29:6 (2 Ne. 27:2). Bwana atakuja na moto, Isa. 66:15. Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha na kuitakasa, Mal. 3:2 (3 Ne. 24:2; M&M 128:24). Atakubatiza kwa Roho Mtakatifu, na kwa moto, Mt. 3:11 (Lk. 3:16). Wenye haki watahifadhiwa kwa moto, 1 Ne. 22:17. Waovu wataangamizwa kwa moto, 2 Ne. 30:10. Nefi alielezea namna gani tunapokea ubatizo wa moto na Roho Mtakatifu, 2 Ne. 31:13–14 (3 Ne. 9:20; 12:1; 19:13; Eth. 12:14; M&M 33:11). Utatangaza msamaha wa dhambi kwa ubatizo, na kwa moto, M&M 19:31. Kanisa kuu na lenye kuchukiza litatupwa chini kwa moto uteketezao, M&M 29:21. Dunia itapita kama vile kwa moto, M&M 43:32. Uwepo wa Bwana utakuwa kama moto uyeyushao, M&M 133:41. Adamu alibatizwa kwa moto na Roho Mtakatifu, Musa 6:66.