Kifo cha kishahidi, Mfiadini Mtu aliye tayari kufa kuliko kumtupa Kristo, injili, au imani yake ya uadilifu au kanuni. Damu zote za haki tangu Abeli hadi Zakaria zitashuhudia dhidi ya uovu, Mt. 23:35 (Lk. 11:50). Mtu yeyote atakayeupoteza uhai wake kwa ajili ya Kristo na injili ataokolewa, Mk. 8:35 (M&M 98:13). Nao walimtupia mawe Stefano, Mdo. 7:59 (Mdo. 22:20). Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo na mauti yake aliyelifanya, Ebr. 9:16–17. Abinadi alianguka, akiwa amekufa kwa moto, Mos. 17:20. Waamoniha walioongoka walitupwa katika moto, Alma 14:8–11. Wengi waliuawa kwa sababu walishuhudia juu ya mambo haya, 3 Ne. 10:15. Mtu yeyote autoaye uhai wake katika kazi yangu atapata uzima wa milele, M&M 98:13–14. Joseph Smith na Hyrum Smith walikufa kifo cha kishahidi kwa urejesho wa injili, M&M 135. Joseph Smith alitia muhuri ushuhuda wake kwa damu yake, M&M 136:39.